AMANA BANK YAZINDUA PROGRAMU YA KIDIGITALI INAYOWEZESHA HUDUMA ZA KIISLAMU
Wafanyakazi wa Benki ya Amana wakijaribu matumuzi ya Apps hiyo wakati wa uzinduzi wa programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama Amana Bank App ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni. *** Wakati taasisi za kifedha zinaendelea kubadilika na kurahisisha huduma na njia ya kufanya biashara, Amana Bank imetangaza kuzindua programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama Amana Bank App ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni. Amana Bank Limited, inayoongoza kwa kutoa huduma za Kibenki za Kiisilamu nchini Tanzania, leo imetangaza kuwa imefanya mapinduzi ya huduma zake za kibenki kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha programu mpya kupitia simu za mkononi, inayomwezesha mteja kufanya malipo na huduma za kibenki kwa wateja wake iitwayo Amana Bank App ; Programu inawezesha kupata huduma za kibenki kidigitali kama vile kufanya malipo, kuhamisha fedha, kulipa bili na kufanya malipo mtandaoni, kupo...