Posts

AMANA BANK YAZINDUA PROGRAMU YA KIDIGITALI INAYOWEZESHA HUDUMA ZA KIISLAMU

Image
  Wafanyakazi wa Benki ya Amana wakijaribu matumuzi ya Apps hiyo wakati wa uzinduzi  wa programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama  Amana Bank App  ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni. *** Wakati taasisi za kifedha zinaendelea kubadilika na kurahisisha huduma na njia ya kufanya biashara, Amana Bank imetangaza kuzindua programu yake mpya ya kidigitali ijulikanayo kama  Amana Bank App  ambayo itawawezesha wateja kufanya miamala mtandaoni. Amana Bank Limited, inayoongoza kwa kutoa huduma za Kibenki za Kiisilamu nchini Tanzania,  leo imetangaza kuwa imefanya mapinduzi ya huduma zake za kibenki kupitia simu za mkononi kwa kuanzisha programu mpya kupitia simu za mkononi, inayomwezesha mteja kufanya malipo na huduma za kibenki kwa wateja wake iitwayo  Amana Bank App ; Programu inawezesha kupata huduma za kibenki kidigitali kama vile kufanya malipo, kuhamisha fedha, kulipa bili  na kufanya malipo mtandaoni, kupo...

Serikali Kuhakikisha Mawasiliano Ya Utangazaji Yanafika Kote nchini

Image
  Na Prisca Ulomi, WMTH Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile amesema kuwa Serikali itahakikisha mawasiliano ya utangazaji yanafika kote nchini kwa kuwa mawasiliano ya redio yanawapata taarifa mbali mbali wananchi na Wizara tunapenda kuona maudhui ambayo yanaendana na utamaduni wetu Tanzania na yanajibu changamoto za wananchi kwa kuwa sasa kuna taarifa ambazo sio sahihi zinatolewa kwa wananchi kupitia baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii. Ameongeza kuwa Serikali itapunguza gharama za leseni za redio jamii na za pembezoni zilizopo ngazi ya Wilaya ili kuondoa adha ya wananchi waishio pembezoni mwa mipaka ya nchi yetu kwa kusikiliza redio za nchi nyingine za jirani Dkt. Ndugulile ameyasema hayo jana akiwa Mgeni Rasmi kwenye uzinduzi na makabidhiano ya studio ya kisasa ya kidijitali ya TBC ya redio jamii ya Mjini Dodoma kwa kuwa ukarabati, ununuzi na ufungaji wa mitambo ya studio hiyo umegharamiwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) a...

SUZA : NJOONI KWENYE BANDA LETU KWENYE MAONYESHO YA TCU

Image
   Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewakaribisha na kuwashauri  wananchi wakiwemo wazazi walezi kutembelea banda lao la Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia Vyuo Vikuu wapatiwe maelekezo sahihi ya kozi zitolewazo na chuo hicho ili waweze kuwashauri watoto wao taaluma bora za kusoma katika mwaka wa masomo wa 2021/22. Aidha, chuo hicho kimewakaribisha wanafunzi waliomaliza kidato cha sita kufika katika banda lao ili wapatiwe maelekezo ya kufanya udahili kutoka kwa wataalamu na taaluma bora za kusoma zinazofundishwa na SUZA. Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam  katika Viwanja vya Mnazi Mmoja kwenye uzinduzi wa maonesho hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) na Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa SUZA, Khadija Sadiq Mahumba. Amesesma wazazi wataofika katika banda lao watapatiwa elimu bora ya namna ya kuchagua kozi zinazowafaa watoto huku akibainisha wanafunzi watapatiwa elimu bora ya namna ya kuchagua kozi zinazowafaa kw...

PROF. MANYA AJIONEA MAAJABU YA CHUO CHA VETA KWENYE MAONESHO YA BIASHARA NA TEKNOLOJIA YA MADINI SHINYANGA

Image
  Kushoto ni Mwalimu wa Chuo cha Ufundi Veta Shinyanga, Robert Onesmo akimwelezea Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya (katikati) kuhusu madini yaliyokatwa na kung'arishwa na kutengenezwa mapambo na urembo katika Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga. Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea Banda la Chuo cha Ufundi Stadi VETA mkoa wa Shinyanga kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Naibu Waziri wa Madini Prof. Shukrani Manya ametembelea banda hilo la Chuo cha Veta wakati akifungua Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Jumapili Julai 25,2021. Akiwa katika banda la Chuo cha VETA Shinyanga, Prof. Manya amejionea fani mbalimbali zinazotolewa katika chuo ikiwemo Fani ya ...

AWLN KWA KUSHIRIKIANA NA TAASISI YA MWALIMU NYERERE ZAPEWA CHANGAMOTO YA KUSIMAMIA AMANI AFRIKA

Image
  Na Mwandishi wetu, Dar Mtandao wa Uongozi wa Wanawake Afrika (AWLN) kwa kushirikiana na Taasisi ya Mwalimu Nyerere umepewa changamoto ya kukuza na kusimamia masuala ya umoja na amani katika Bara la Afrika ili kuleta maendeleo ya watu.   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ametoa wito huo wakati alipokutana na Mtandao huo pamoja na Taasisi ya Mwalimu Nyerere ikishirikiana na Shirika la Kimataifa la kutetea Haki na Maendeleo ya Wanawake (UN Women) leo jijini Dar es Salaam “Agenda yetu ni muhimu, hamuwezi kusema kuwa tuna maendeleo kama hakuna amani…….amani ni sehemu ya Diplomasia ya Uchumi, kama amani huwezi kuitafuta kwa njia nyingine tuseme amani ni maendeleo na maendeleo ni amani,” Amesema Balozi Mulamula Balozi Mulamula ameongeza kuwa, kwa kuzingatia kwamba amani ni matokeo ya haki juhudi zinahitajika katika kuhamasisha na kuunga mkono ushiriki kamili wa wanawake kama wadau muhimu wa kulinda na kutetea amani. Kwa upande wake, ...

WAZIRI MKUU APOKEA TAARIFA YA KAMATI YA MOTO SOKO LA KARIAKOO

Image
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo, Julai 27, 2021 amepokea taarifa ya Kamati ya   Uchunguzi wa tukio la moto uliotokea katika soko la kimataifa la Kariakoo tarehe 10 Julai, 2021 jijini Dar es salaam. Mheshimiwa Majaliwa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa mwenyekiti wa Kamati  hayo, CP Liberati Sabas na kuahihidi kuwa serikali itayafanyia kazi mapendekezo yote yaliyotolkewa na Kamati hiyo.   Akizungumza baada ya kuipokea taarifa hiyo kwenye Makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es salaam, Mheshimiwa Majaliwa    amewashukuru na amewapongeza wajumbe wa Tume hiyo kwa kazi nzuri iliyofanyika kwa weledi mkubwa.   Mheshimiwa Majaliwa amesema ataifikisha  taarifa hiyo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwani tukio hilo limewagusa watu ndani na nje ya nchi.   “Naahidi mbele yako Mwenyekiti kuwa Serikali imeridhishwa na taarifa mlioyo nikabidhi leo na mapendekeso yote mliyoyato...

TAKUKURU YAANZA KUCHUNGUZA MABILIONI YA FEDHA MANISPAA YA SHINYANGA

Image
  Mkuu wa TAKUKURU mkoani Shinyanga Hussen Mussa akitoa taarifa kwa vyombo vya Habari. Na Mwandishi wetu, Shinyanga. TAASISI ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Shinyanga, imeanza kuchunguza matumizi ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 31.161 zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB) kwa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Shinyanga, Hussein Mussa uchunguzi huo unatokana na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa hivi karibuni. Mussa amesema, katika ukaguzi maalumu uliofanywa na CAG ilibainika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ilipokea jumla ya sh, bilioni 31,1kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo, kiasi cha sh. bilioni 26,1 ni fedha zilizotolewa na Benki ya Dunia na sh. bilioni 4,9 kutoka vyanzo vingine. Alisema kutokana na taarifa ya ukaguzi maalumu kwa kipindi cha miaka mitatu imeonekana kuna mapungufu katika matumizi ya fedha hizo kwenye utekelezaji wa...